Polisi wanawasaka wakurugenzi wa hoteli ya Sunstar iliyoporomoka katika kaunti ya Murang’a

Serikali inawatafuta wamiliki watatu wa hotel Sunstar iliyoporomoka siku ya Ijumaa alasiri katika eneo la Gatanga kaunti ya Murang’a.

Mrakibu wa eneo la Kati Wilfred Nyanwanga, ameamuru kukamatwa kwa wakurugenzi watatu wa hoteli hiyo na watu wengine sita ambao hawajulikani waliko.

Akihutubia wanahabari katika eneo hilo, Nyagwanga aliwahimiza washukiwa hao kujisalimisha na kusaidia polisi katika uchunguzi wao.

Also Read
Tume Huru Ya Uchaguzi Yasema Iko Tayari kwa Uchaguzi wa Jumanne

Maafisa wanaamini kuwa kuna watu sita zaidi ambao wangali wamekwama kwenye vifusi vya jengo hilo la horofa nne. Nyagwanga anasema jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi duni.

Wakati huo huo, miili mitatu imefukuliwa kutoka kwenye vifusi vya jumba hilo. Serikali inaamini kuna miili mitano zaidi imenaswa kwenye vifusi vya jumba hilo lenye ghorofa nne lililoporomoka Ijuma alasiri.

Also Read
Msimamizi wa bajeti asema hapingi rukuzu ya gari kwa wawakilishi wodi

Nyangwanga anahusisha kuporomoka kwa jumba hilo na utepetevu wa kitaaluma. Alisema wanakandarasi walikuwa wakitumia vyuma hafifu ambavyo ni vya kiwango cha Y10 kuunganisha kuta,badala ya kutumia vya kiwango cha Y16,jambo ambalo linazua dukuduku kuhusu uhalali wa ujenzi wa jumba hilo.

Also Read
Shule moja yafungwa kaunti ya Kitui kutokana na maambukizi ya Covid-19

Gavana wa Murang’a, Mwangi Wa Iria, amelaumu Halmashauri ya kuu inayosimamia ujenzi kwa kughairi majukumu yake ya kukagua ujenzi unaoendelea kufanywa nchini.

Wa Iria alidokeza kwamba jumba hilo halingeporomoka,wataalam wa halmashauri hiyo wangewajibika katika majukumu yao kisawasawa.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi