Polisi watekwa nyara na Tusker, Ulinzi watoshana ngvu na Gor ligi kuu FKF

Polisi Fc walipoteza uongozi na kushindwa mabao 1-2 na mabingwa watetezi Tusker Fc,  katika pambano la ligi kuu FKF lililosakatwa Jumatano katika uwanja  mdogo wa Kasarani.

Samuel Ndung’u aliwaweka maafande uongozini kwa goli la dakika ya kwanza ya mchezo akiunganisha kwa kichwa mkwaju wa Clifton Miheso .

Also Read
Wanariadha waliotimiza masharti pekee wataalikwa kwa majaribio ya kitaifa wiki ijao

 

Polisi ambao wapoteza mechi 3 kati ya nne za ufunguzi walishindwa kudumisha uongozi na kuwarusu wageni Tusker kusawazisha katika dakika ya 11 kwa bao lake Ibrahim Joshua naye Shami Kibwana akoangeza la pili kupitia mkwaju wa penati na kuenda mapumzikoni kwa uongozi wa 2-1 .

Also Read
Mashemeji waogopana ligi kuu FKF

Ushindi unaipaisha Tusker Fc hadi nafasi ya 10 ligini ukiwa ushindi wa pili msimu huu baada ya mechi 4 ,huku Polisi wakishikilia nafasi ya 14 kwa alama 3.

Also Read
Chipukizi Chebet ashinda nishani ya fedha mita 5,000 mashindano ya riadha duniani Oregon

Katika mchuano mwingine uliosakatwa uwanjani Thika wanajeshi Ulinzi Stars na Gor Mahia walitoka sare tasa .


Gor wanaongza jedwali kwa alama 13,  kutokana na mechi tano wakifuatwa na Kakamega Homeboyz na Bandari FC kwa alama 12 kila moja.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Kenya kukabana koo na Puerto Rico mechi ya mwisho ya kundi A mashindano ya dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi