Polycarp Igathe Akubali Matokeo ya Uchaguzi wa Ugavana Nairobi

Polycarp Igateh ambaye alikuwa anawania wadhifa wa ugavana katika kaunti ya Nairobi kupitia chama cha Jubilee chini ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya amekubali matokeo ambayo yametangazwa asubuhi ya leo ambapo alibwagwa na Johnson Sakaja wa chama cha UDA katika kinyang’anyiro hicho.

Also Read
Kaunti zatakiwa kuongoza vita dhidi ya COVID-19

Kupitia Twitter Igathe amesema anakubali uamuzi wa watu wa Nairobi na akashukuru wafuasi wake wote. “Gavana wa Nairobi ni Johnson Sakaja. Pongezi! Mungu abariki Kenya” ndiyo baadhi ya maneno ambayo Igathe ameandika kwenye Twitter.

Also Read
Ujumbe Wa EAC Waridhishwa na Usimamizi wa Uchaguzi Nchini

Sakaja alijizolea kura 669,392 huku Igathe akijipatia kura 573,516. Nyadhifa nyingine mbili za kiwango cha kaunti katika kaunti ya Nairobi ambazo ni mwakilishi wa kike bungeni na seneta zinashikiliwa na chama cha ODM kupitia kwa Esther Muthoni Passaris na Edwin Sifuna mtawalia.

  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi