Stanley Okumbi na Kelvin Opiyo wote kutoka Posta Rangers wameshinda tuzo ya kocha na mchezaji bora katika ligi kuu ya Kenya FKF katika mwezi wa Machi.
Okumbi aliongoza Rangers kushinda mechi mbili na kutoka sare moja mwezi uliopita ikiwemo kwenda sare tasa na Kariobangi Sharks,kabla ya kusajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gor Mahia na kuwalemea Mathare United magoli 2-0.
Okumbi amepokea tuzo na shilingi 50 ,000 huku akiwashinda Nicholas Muyoti wa Kakamega Homeboyz na Emmanuel Vas Pinto wa Gor Mahia.
Opiyo ambaye ni mlinda lango wa Rangers pia alikuwa ngangari huku akikosa kufungwa bao lolote katika mechi tatu za mwezi huo na kuwashinda Alex Ochwari , Wilson Silva ,kiungo Cliffton Miheso, Anthony Kimani, kiungo Christoper Masinza na mshambulizi Peter Lwasa wa Kariobangi Sharks.