Msanii maarufu wa nyimbo za Hip Hop Tanzania Bara Joseph Haule maarufu kama Prof Jay amepoteza ubunge wa Mikumi baada ya kubwagwa na mpinzani wa Chama cha Mapiunduzi CCM.
Prof jay akigombea kiti hicho kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) alipata kura 17,375 dhidi ya mgombea wa chama tawala cha CCM Denis Lazaro aliyeibuka mshindi kwa kupata kura 31,411 .
Prof Jay ameliongoza Jimbo la Mikumi kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda kwenye Uchaguzi uliopita mwaka 2015 .
Uchaguzi mkuu wa Tanzania uliandaliwa Jumatano huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea kwa maeneo mengi nchini humo.