Prof. Magoha asimamisha mabadiliko katika chuo kikuu cha Nairobi

Waziri wa elimu Prof. George Magoha amesimamisha mabadiliko yaliyofanya hivi majuzi katika chuo kikuu cha Nairobi.

Magoha alisema mabadiliko hayo kwanza kabisa yangewasilishwa afisini mwake kupigiwa kurunzi kabla ya kuanza kutekelezwa.

“Mapendekezo hayo ambayo yanaondoa na kubuni nafasi katika uongozi wa chuo kikuu cha umma hasaa yale ambayo hayajajumuishwa katika sheria ya vyuo vikuu ya mwaka 2012, yanaoaswa kuzingatia sheria inayotoa mwongozo kwa mabadiliko hayo,” alisema Magoha.

Also Read
Magoha akosolewa kwa kutotangaza tarehe ya ufunguzi wa shule

Katika barua kwa wenyeviti wa vyuo vikuu na nakala kutumwa kwa mkuu wa utumishi wa umma  Joseph Kinyua na mwanasheria mkuu, Magoha aliagiza mabadiliko hayo kusitishwa mara moja hadi idhini itakapotolewa na mamlaka husika.

Also Read
Magoha ataka vivuli vya miti vitumike kama madarasa, kwani shule sharti zifunguliwe

Magoha alitoa wito kwa vyuo vikuu ambavyo vimetangaza mabadiliko kama vile chuo kikuu cha Nairobi kuwasiliana na afisi yake kuhusu mabadiliko hayo.

Baraza la chuo kikuu cha Nairobi hivi majuzi lilitangaza mabadiliko yaliyojumuisha kuondolewa kwa baadhi ya afisi, kujumuishwa kwa afisi zingine na kubuniwa kwa idara mpya.

Mwenyekiti wa baraza la chuo kikuu cha Nairobi Prof Julia Ojiambo alisema mabadiliko hayo mapya yalitokana na kuboresha mafunzo, uvumbuzi na  utafiti wa chuo hicho kikuu.

Also Read
Rigathi Gachagua anatarajiwa kufikishwa Mahakamani

Hata hivyo magoha alisema mabadiliko hayo kwanza yangewasilishwa afisini mwake kupitia tume ya elimu ya vyuo vikuu kabla ya kutekelezwa kupitia kwa Kamati ya ushauri ya mashirika ya serikali.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi