Prof Magoha: Hakuna mipango ya kufunga shule

Waziri wa Elimu professa George Magoha,amethibitisha kwamba hakuna mipango ya kufunga shule tena licha ya ongezeko la visa vipya vya maambukizi ya Corona.

Waziri aliyasema hayo alipozuru shule mbali mbali katika maeneo ya Mumias na Malaba.

Waziri alisema wanafunzi million 3 wa gredi 4,darasa la nane na kidato cha nne wamerejelea masomo katika awamu ya kwanza ya ufunguzi wa shule.

Also Read
Serikali yatetea hatua ya kufunga barabara ya Thika jana usiku

Akikiri kuwa maambukizi mapya yanaongezeka,waziri alisema wizara ya elimu inashirikiana na ile ya usalama wa kitaifa kufwatilia hali ilivyo.

Kadhalika alipuuzilia mbali madai kwamba wanafunzi katika shule kadhaa wamekosa mjarabu unaoendelea.

Also Read
Visa 485 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Wakati uo huo chama cha shule za kimataifa nchini kimetangaza kufutiliwa mbali kwa mipango ya kufungua shule kwa wanafunzi wote tarehe 26 mwezi huu kama ilivyokuwa imepangwa.

Chama hicho hata hivyo kimesema masomo yataendelea kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho na wale wa gredi zilizofungua tarehe 12 mwezi huu.

Also Read
Watu 490 zaidi wapona Covid-19 huku 143 wakiambukizwa virusi hivyo

Ili kuhakikisha usalama kwa wanafunzi,chama hicho kimehimiza taasisi husika kuzingatia kanuni za kuzuia kusambaa kwa korona zilizotangazwa na wizara ya afya.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi