Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha kwa mara nyingine amewapuuzilia mbali wale wanaokosoa mtaala wa elimu wa (CBC), huku akiutaja kuwa jambo bora zaidi lililowahi kutokea katika mfumo wa elimu hapa nchini.

Huku akisisitiza kwamba mtaala wa elimu wa (CBC), hautapuuzwa, Profesa Magoha alisema inafaa pia ijulikane kwamba sekta ya elimu nchini Kenya imechukua mkondo ufaao kwa kuangazia maarifa na uadilifu wa wanafunzi badala ya kuwaorodhesha wanafunzi na kuwaweka katika mashindano Jinsi ambavyo imeshuhudiwa kwa miaka mingi.

Also Read
Wanasheria nchini wamshinikiza Rais Kenyatta kuteua majaji 41

Mtaala wa elimu wa (CBC), umeshtumiwa vikali na baadhi ya viongozi wa ki-siasa na pia wadau, huku wakidai kwamba ulitekelezwa kwa haraka.

Akiongea Ijumaa wakati alipoongoza hafla ya sita ya kufuzu kwenye chuo kikuu cha Embu ambako mahafali 1,570 walitunikiwa Stashahada na Shahada katika nyanja mbali mbali, Magoha alisema mtu yeyote asi-jichukulie kuwa shujaa kuhusiana na utaratibu uliokusudiwa kubadili mfumo wa elimu hapa nchini.

Also Read
Magoha: Serikali iko tayari kutekeleza mtaala wa CBC

Rais wa chama cha wana-sheria humu nchini-(LSK), Nelson Havi, tayari amewasilisha rufaa mahakamani kupinga mtaala wa huo wa CBC.

Also Read
Marekani kuisaidia kaunti ya Mombasa kuboresha utoaji wa huduma

Prof. Magoha hata hivyo alitoa wito wa kuto-ingizwa siasa katika sekta ya elimu huku alielezea kuwa hakuna kurudi nyuma kuhusu mfumo mpya wa elimu.

“Hakuna watoto ambao ni wa chama fulani cha kisiasa, Kwa hivyo ni bora kuondoa siasa katika sekta ya elimu,” alisema Magoha.

  

Latest posts

Kliniki mpya ya ugonjwa wa saratani yafunguliwa katika kaunti ya Nandi

Tom Mathinji

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi