Rachier airai wizara ya michezo kuinusuru Gor Mahia FC kupitia Sports Fund

Mwenyekiti wa Gor Mahia FC  Ambrose Rachier ameirai wizara ya michezo kuingilia kati mapema na kuinusuru timu hiyo kifefha kupitia hazina ya kitaifa ya michezo yaani national sports fund.

Gor-Mahia

Rachier amesisitiza kuwa timu hiyo haina  uwezo wa kifedha kugharamia mechi za msimu ujao za kombe la shirikisho la soka CAF .

Also Read
KBC Channel One kuonyesha mechi ya Kenya dhidi ya Comoros Jumatano

“Ukweli ni kuwa kama tungekuwa na uwezo tungejiondoa lakini pia kukiondoa kutaigharimu timu zaidi kwani huenda tukapigwa faini na kufungiwa kushiriki mashindano.
Kila msimu tumekuwa na matatizo wakati wa mechi hizi ,kwani ziara ya mechi moja kwenda Afrika kaskazini inatugharimu shilingi milioni 6 kila safari kulipia tiketi za ndege ,bado tunaomba serikali kupitia hazina ya michezo kutoa msaada wao kwa timu kwa wakati unaofaa”akasema Rachier

Also Read
Tusker FC warejeshwa tena kazkazini mwa Afrika dhidi ya CS Faxien Gor wakikutana na Otoho
Also Read
Wakulima wahimizwa kununua pembejeo za kilimo kwa wauzaji waliosajiliwa

Gor itaanza kampeini za kushiriki kombe la shirikisho mwezi Septemba mwaka huu.

 

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier-(c)Jackson Mnyamwezi

Tusker Fc wataiwakilisha Kenya katika ligi ya mabingwa Afrika michuano ya mchujo pia iking’oa nanga Septemba.

  

Latest posts

Bodi ya dawa na sumu yapiga marufuku uuzaji wa dawa ya kupanga uzazi ya ‘Sophia’

Tom Mathinji

Bunge la kitaifa na la Seneti kuanza vikao vyao Jumanne

Tom Mathinji

Sharon Chepchumba atua Ugiriki kupiga Voliboli ya kulipwa kwa miezi sita

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi