Raia 22 watiwa nguvuni kwa kuingia hapa nchini kinyume cha sheria

Maafisa wa polisi katika mji wa Maralal wamewatia nguvuni wahamiaji 22 haramu ambao ni raia wa nchi jirani ya Ethiopia.

Kulingana na maafisa wa polisi wahamiaji hao walikuwa wakisafiri wakitumia gari aina la Toyota Land Cruiser lenye nambari za usajili KCU 595H wakati walipokamatwa kwenye barabara kati ya Opiroi na Maralal.

Also Read
Wakenya watahadharishwa kuhusu mafuriko kutokana na mvua kubwa itarajiwayo

Akidhibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi wa Samburu ya kati Sylvester Rotich alisema wanawake 12, wanaume 10 na mtoto mmoja wa umri wa miezi tisa, walikuwa kwenye gari hilo la kijani kibichi.

“Gari hilo lilisimamishwa na maafisa wa polisi katika barabara ya Oporoi na baada ya kukaguliwa, polisi waliwapata watu hao ambao hawakuwa na stakabadhi na hawangeweza kuzungumza kingereza au kiswahili,” alisema Rotich.

Also Read
Tume ya usawa na jinsia yataka sheria kupitishwa kukabiliana na dhuluma za kijinsia

Rotich alisema gari hilo lilitoka eneo la Moyale kwenye mpaka kati ya Kenya na Ethiopia na walikuwa wakisafiri wakielekea Nairobi.

“Watu hao 22 pamoja na dereva wao raia wa Kenya wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mararal wakisubiri kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kuwa humu nchini kinyume cha sheria,” aliongeza Rotich.

Also Read
Watu wawili wauawa kwa kupigwa risasi Baragoi

Kamanda huyo wa polisi alitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kuripoti gari lolote wanalolishuku na ambalo lina watu wasiojulikana.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi