Raia wa Kenya na Sudan Kusini hawahitaji Visa kuingia nchi hizo

Kenya na Sudan Kusini zimeondolea mbali masharti ya visa kwa wananchi wao wanaonuia kusafiri katika mataifa hayo mawili.

Kupitia kwa taarifa katika vyumba vya habari, katibu katika wizara ya mashauri ya kigeni balozi Macharia Kamau, alisema kuondolewa kwa masharti hayo ya kusafiri kunaanza kutekelezwa mara moja.

Also Read
Soko jipya la Githurai lakumbwa na utata wa ugavi wa vibanda

“Jamuhuri ya Kenya imeondoa masharti ya kupata visa kuingia hapa nchini kwa raia wa Sudan Kusini wanaomiliki pasipoti zilizotolewa na serikali ya Sudan Kusini,” alisema balozi huyo.

Zaidi ya hayo, kuambatana na sehemu ya 10 ya taratibu za soko la jumuia ya Afrika Mashariki, wafanyikazi kutoka kwa mataifa hayo mawili wanakubaliwa kuajiriwa katika nchi hizo mbili.

Also Read
Morans wapakatwa na Angola michuano ya kufuzu kwa Fiba Afrobasket

Alisema kuondolewa huko kwa visa, kunaashiria ushirikiano dhabiti kati ya serikali ya Kenya na Ile ya Sudan Kusini.

Vile vile hatua hiyo inakusudia kuboresha uhusiano wa kitamaduni na kuimarisha chumi za mataifa haya mawili kwa kuruhusu usafirishaji wa watu na nguvukazi , hii ikiwa nguzo muhimu katika utangamano wa jamii ya Afrika Mashariki.

Also Read
Rais Kenyatta na Suluhu waahidi kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya Kenya na Tanzania

Kenya na Sudan Kusini zinatarajiwa kutia saini mkataba wa maelewano kuhusu swala hili hivi karibuni.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi