Raia wa Palestina wamuomboleza mwanahabari Shireen Abu Akleh

Serikali ya Palestina imeandaa ibada ya wafu ya kitaifa kwa mwanahabari aliyeuawa wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh alioyeuawa na maofisa wa usalama wa Israeli.

Familia na marafiki leo adhuhuri wamemuomboleza mwendazake huku mamia ya wapalestina wakijumuika kumuomboleza.

Also Read
Kesi ya ufisadi dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kurejelewa

Wanajeshi wa Israeli walimuua kwa kumpiga risasi mwanahabari huyo katika eneo linalozozaniwa na ukingo wa magharibi kulingana na wizara ya afya ya Palestina.

Akleh, ambaye amelifanyia kazi kwa miaka mingi shirika la habari la Al Jazeera aliuawa jana akipokuwa akiangazia uvamizi wa vikosi vya Israeli katika mji wa Jenin.

Also Read
Mwanamke wa kwanza ateuliwa katibu wa kijeshi kwa Afisi ya Rais nchini Israel

Mwanahabari mwingine wa Al Jazeera Ali al-Samoudi,alipata majeraha ya risasi mgongoni japo yuko katika hali dhabiti.

Also Read
Idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko nchini Indonesia na Timor yafikia 71

Picha za video zimeonesha mwanahabari huyo alifariki baada ya kupigwa risasi kichwani.

Aidha marehemu mzaliwa wa Jerusalem amekuwa mwanahabari tajika ambaye amehusika katika uangaziaji wa vita baina ya Israeli na Palestina kwa miaka mingi.

  

Latest posts

Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Tom Mathinji

Biashara ya bidhaa za Afrika kwa njia ya mtandao wa Internet kupanua mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China

Tom Mathinji

Ushirikiano kati ya China na Afrika unawasaidia watu wa Afrika kukabiliana na changamoto zao za kimaisha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi