Raia wa Sudan warejelea maandamano kupinga utawala wa kijeshi

Waandamanaji nchini Sudan wameanzisha tena maandamano barabarani kulalamikia utawala wa kijeshi ambao umekuwa ukiongoza nchi hiyo huku wakitoa wito wa kubuniwa kwa serikali ya kiraia.

Umati mkubwa wa watu ulionekana karibu na ikulu ya rais jijini Khartoum kufuatia miito ya makundi kadhaa ya wale wanaopinga utawala huo.

Also Read
Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Hii ndio idadi kubwa zaidi ya watu kuwahi kujitokeza tangu mwezi mtukufu wa Ramadhan nchini humo.

Haya yamejiri huku wanaharakati wakishtumu hatua ya vikosi vya usalama kutumia risasi na gesi ya kutoza machozi wakati wa makabiliano na waandamanaji ambayo yamesababisha vifo na majeraha mabaya.

Also Read
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir avunja bunge la nchi hiyo

Mawakili nchini humo wamesema kuwa zaidi ya waandamanaji 80 wa kisiasa wangali wanazuiliwa gerezani ambao wengi wao wanateswa.

Also Read
Serikali ya Sudan yatia saini mkataba wa Amani na viongozi wa Waasi

Jeshi lilitwaa mamlaka mwezi Oktoba mwaka 2021,  na kukomesha matumaini ya mpito wa kidemokrasia baada ya maasi yaliyodumu kwa miezi kadhaa yaliyomng’atua mamlakani kiongozi wa kiimla Omar al-Bashir.

  

Latest posts

Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Tom Mathinji

Biashara ya bidhaa za Afrika kwa njia ya mtandao wa Internet kupanua mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China

Tom Mathinji

Ushirikiano kati ya China na Afrika unawasaidia watu wa Afrika kukabiliana na changamoto zao za kimaisha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi