Raila akosoa makadirio ya IEBC ya shilingi bilioni 14 kuandaa kura ya BBI

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amepuuzilia mbali madai ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kwamba kura ya maamuzi ya mpango wa BBI inaweza kugharimu shilingi bilioni 14.

Odinga sasa anatoa wito wa kubadilishwa kabisa kwa Tume hiyo pamoja na usimamizi kamili wa uchaguzi humu nchini.

Kwenye taarifa, Waziri Mkuu huyo wa zamani amesema kundi litabuniwa hivi karibuni kujadiliana na tume ya IEBC kuhusu jinsi ya kuandaa kura ya maamuzi na chaguzi za gharama ya chini.

Also Read
Kaunti ya Elgeyo Marakwet yaangusha mswada wa BBI

Kulingana na Odinga, chaguzi za humu nchini zimekuwa zikitumiwa kupora mali ya umma.

Kiongozi huyo wa Chama cha ODM amesema katika mataifa yaliyostawi kidemokrasia, ambayo huandaa chaguzi mara kwa mara, gharama ya uchaguzi kwa kila mpiga kura ni kati ya shilingi 100 na 200.

Also Read
Hosea Kiplagat ambaye ni msaidizi wa zamani wa Rais Moi amefariki

Odinga amehoji kuwa kwa sababu Kenya ina taasisi bora zikiwemo vituo vya polisi, shule, afisi za serikali na miundo mbinu bora ya uchukuzi, gharama ya kuandaa kura ya maamuzi itakuwa chini ya shilingi bilioni mbili.

Amesema ripoti ya maridhiano ya kitaifa BBI inanuiwa, miongoni mwa masuala mengine, kukabiliana na ufisadi na kuhakikisha uadilifu kwenye taratibu za uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwianisha gharama kufikia zile za kimataifa.

Also Read
Rais Kenyatta afungua rasmi barabara mpya

“Hali hii ya kutojali haifai kuruhusiwa kuathiri zoezi la kura ya maamuzi ya BBI yenye malengo ambayo ni pamoja na kusitisha tabia ya wizi wa rasilimali za umma na ufisadi katika afisi za umma,” amesema Odinga.

Haya yanajiri baada ya tume ya IEBC kuwaambia wabunge kuwa kura hiyo itagharimu takribani shilingi bilioni 14 kwa makadirio.

  

Latest posts

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Watu wawili wafariki baada ya mashua kuzama Homa Bay

Tom Mathinji

Bunge lachunguza nyongeza ya bei za mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi