Raila ashinikizwa kujiunga na One Kenya Alliance

Viongozi wa chama cha Ford Kenya wametoa changamoto kwa kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga, kujiunga na muungano wa  One Kenya Alliance kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Huku ikiwa imesalia mwaka mmoja kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu hapa nchini, viongozi hao wa chama cha FORD Kenya, walisema  Raila Odinga atashindwa na naibu Rais William Ruto ikiwa hataungwa mkono na muungano wa One Kenya Alliance.

Also Read
KeNHA yakabili msongamano wa magari unaosababishwa na ujenzi wa barabara ya moja kwa moja Nairobi

Haya yanajiri baada ya kiongozi wa ANC  Musalia Mudavadi, Yule wa FORD-Kenya Moses Wetangula na mwenzao wa Wiper  Kalonzo Musyoka kutengana na waziri mkuu huyo wa zamani miezi michache tu baada ya Raila kuafikiana na Rais Uhuru Kenyatta huku viongozi hao watatu wakiungana na kiongozi wa chama cha KANU Gideon Moi.

Wakiongozwa na mbunge wa Kwanza Ferdinand Wanyonyi, viongozi hao wa Ford Kenya  walisema wanamkaribisha  Raila Odinga kwa muungano huo wa One Kenya Alliance ili kubuni muungano wa kisiasa utakaowawezesha kumrithi Rais  Uhuru Kenyatta.

Also Read
Watu 497 zaidi waambukizwa Corona huku wagonjwa 16 wakiaga dunia

Akizungumza mjini Kitale baada ya kuzindua zoezi la kuwasajili wanachama,  viongozi hao walisema One Kenya Alliance utabuni serikali ijayo huku wakimshauri Raila Odinga kuungana nao kwa majadiliano ya kumtafuta atakayepeperusha bendera ya muungano huo katika uchaguzi mkuu ujao.

Kulingana na Wanyonyi iwapo Raila atakosa kujiunga na muungano huo na kuwania urais peke yake katika uchaguzi mkuu ujao, basi atapoteza kiti hicho kwa naibu rais Dkt William Ruto.

Also Read
Kaunti ya Makueni kuhakikisha wanafunzi wote wanarejea shuleni mwakani

Wanyonyi alisema muungano wa One Kenya utawaunganisha wakenya wote kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Alitoa wito kwa wakenya kuwapuuza viongozi wanaowagawanya wakenya kwa misingi ya kikabila.

Wanyonyi alisema Ford Kenya imezindua zoezi la kuwasajili wanachama ili kuongeza idadi ya wanachama wake kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

  

Latest posts

Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tom Mathinji

Mudavadi asema taifa hili halipaswi kushuhudia ghasia kama zile za mwaka 2007

Tom Mathinji

Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi