Raila atoa wito kwa viongozi wanawake kuunga mkono BBI

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema kuwa ripoti ya BBI inalenga kuwaweka wanaume na wanawake walio kwenye ulingo wa siasa katika kiwango sawa.

Raila alisema kuwa kupitia kwa ripoti hiyo, taifa hili litaweza kuafikia sheria ya thuluthi mbili katika maswala ya jinsia.

Also Read
Kijana aliyemkata kichwa nyanyake kuzuiliwa korokoroni kwa siku saba zaidi

Raila ambaye alikuwa akiwahutubia viongozi wa wanawake wa mashinani katika kaunti ya Nairobi, alitoa wito kwao kupigia debe ripoti hiyo kwa vile watanufaika pakubwa iwapo itaungwa mkono na kuidhinishwa na wakenya.

Also Read
Rais Kenyatta: Ushirikiano thabiti wa kimataifa ni nguzo muhimu kukabiliana na changamoto zilizopo

Kwa mara nyingine alishtumu kampeini tata zinazolenga kuhujumu mchakato huo huku akitoa wito kwa viongozi wa kike kuiunga mkono.

Alikashifu matamshi yanayohusishwa na upande unaomuunga mkono naibu wa Rais  William Ruto ambao unadai kuwa mchakato wa  BBI si swala muhimu kwa sasa.

Also Read
Kadi za Huduma Namba ziko tayari kusambaziwa wakenya

Kwa mujibu wa Raila, naibu wa rais na washirika wake hawaambii wakenya ukweli.

Alisisitiza kuwa ripoti ya BBI ndio zawadi bora  ambayo yeye na rais  Uhuru Kenyatta wanaweza kukabidhi kwa kizazi kijacho.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi