Raila atoa wito wa kustawishwa Viwanda katika sehemu za mashinani

Kinara wa ODM, Raila Odinga ametoa wito wa kufadhili maarifa ya humu nchini na ustawi wa kiviwanda katika sehemu za mashinani ili kuboresha mipango ya kuzalisha bidhaa za humu nchini.

Raila alisema WaKenya wanaweza kuwa na bidhaa bora zilizotengenezewa humu nchini iwapo serikali itaangazia mabadiliko katika sehemu za mashinani na kukuza vipaji.

Also Read
Ruto alaumu ODM kwa kuhujumu ajenda ya Jubilee

Raila ambaye aliitaja kaunti ya Kwale kuwa mfano bora, alisema wakazi wa eneo hilo hutumia maarifa yao wenyewe kuzalisha Tui na mafuta tosha ya Mnazi kwa matumizi yao ya nyumbani.

Hata hivyo alisema kukiwa na usaidizi wowote wa kuboresha maarifa ya kiasili, nchi hii itakuwa na kiwanda kinachomilikiwa na WaKenya cha kuzalisha Tui na mafuta ya Mnazi kwa gharama nafuu.

Also Read
Hoja ya kumng'atua Spika wa kaunti ya Tana River yaidhinishwa

Kupitia taarifa ya kitandazi cha twitter, Raila alisema katika siku zijazo, uwekezaji katika vipaji na mabadiliko ya sehemu za mashinani kwa ajili ya ustawi wa kiviwanda litakuwa jambo muhimu.

Also Read
Muda wa kafyu waongezwa huku mikutano ya hadhara ikipigwa marufuku

kiongozi huyo wa ODM aliongeza kwamba kila eneo la humu nchini limebarikiwa na mazao ambayo yanahitaji uwekezaji fulani katika maarifa ya wakazi na pia miundo msingi ya mashinani ili kubadili maisha ya wakenya.

  

Latest posts

Chissano atoa wito wa mazungumzo kati ya serikali na wapiganaji

Tom Mathinji

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi