Raila awaonya Wakenya dhidi ya ‘kuhadaiwa tena na Ruto’

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kile alichokitaja kuwa kuhadaiwa kwa mara ya pili na Naibu Rais William Ruto na wandani wake.

Raila amesema kabla ya kuchaguliwa kwake, Ruto aliwahidi Wakenya mambo mengi, ila serikali anayohudumu haijafanikiwa kutimiza ahadi hizo.

Also Read
Bunge la Kitafa na lile la Senate zatakiwa kusuluhisha tofauti baina yazo

Raila anashangazwa na jinsi Naibu Rais anazidi kuwapa Wakenya ahadi za endapo atachaguliwa kuwa rais mwaka wa 2022, ilhali hajatekeleza ahadi alizotoa awali kabla ya kuwa naibu rais.

Also Read
IEBC yaidhinisha mswada wa BBI

Kiongozi huyo wa ODM amesema hayo baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa moja la Katoliki katika mtaa wa Soweto, Eneo Bunge la Embakasi, ambako amewarai waumini kuunga mkono mchakato wa BBI.

Also Read
Odinga: Siwanii kuungwa mkono katika uchaguzi mkuu ujao

Raila amesema maslahi ya makanisa yamenakiliwa vizuri kwenye ripoti ya BBI, baada ya mashauriano ya kina baina ya wana kamati wa BBI na wawakilishi wa makanisa.

Aidha, Raila amewashtumu wanaopinga ripoti hiyo, akiwataja kuwa wanafiki.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi