Raila awaonya Wakenya dhidi ya ‘kuhadaiwa tena na Ruto’

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewatahadharisha Wakenya dhidi ya kile alichokitaja kuwa kuhadaiwa kwa mara ya pili na Naibu Rais William Ruto na wandani wake.

Raila amesema kabla ya kuchaguliwa kwake, Ruto aliwahidi Wakenya mambo mengi, ila serikali anayohudumu haijafanikiwa kutimiza ahadi hizo.

Also Read
Rais Kenyatta awasili Ukambani kukagua Miradi ya maendelo

Raila anashangazwa na jinsi Naibu Rais anazidi kuwapa Wakenya ahadi za endapo atachaguliwa kuwa rais mwaka wa 2022, ilhali hajatekeleza ahadi alizotoa awali kabla ya kuwa naibu rais.

Also Read
Alice Wahome na Ndindi Nyoro wakaidi maagizo ya polisi

Kiongozi huyo wa ODM amesema hayo baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa moja la Katoliki katika mtaa wa Soweto, Eneo Bunge la Embakasi, ambako amewarai waumini kuunga mkono mchakato wa BBI.

Also Read
Raila hategemei kuidhinishwa na Uhuru ili kugombea urais, wasema baadhi ya viongozi wa ODM

Raila amesema maslahi ya makanisa yamenakiliwa vizuri kwenye ripoti ya BBI, baada ya mashauriano ya kina baina ya wana kamati wa BBI na wawakilishi wa makanisa.

Aidha, Raila amewashtumu wanaopinga ripoti hiyo, akiwataja kuwa wanafiki.

  

Latest posts

Uhaba wa maji wakumba kaunti ndogo ya Lagdera baada ya kukauka kwa vidimbwi

Tom Mathinji

Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Tom Mathinji

Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi