Raila awarai wakazi wa Mlima Kenya kuunga mkono azma yake ya kuwania urais

Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga,amesema atatoa uongozi utakaoiwezesha nchi hii kupiga hatua kubwa kiuchumi iwapo atapewa fursa ya kuiongoza nchi hii.

Raila amekariri kwamba uongozi mbaya umepoteza matumaini ya wakenya wengi akiongeza kusema matumaini na ufanisi vinaweza tu kupatikana iwapo tutapambana na magonjwa,kutofahamu, umasikini na uongozi mbaya.

Also Read
Mwenyekiti wa shirika la KBC David Were aifariji familia ya marehemu Justus Murunga

Akiongea na wananchi baada ya kuhudhuria ibada ya jumapili katika kanisa la PCEA mjini Nanyuki, katika kaunti ya Laikipia, kiongozi huyo wa ODM alisema kuwa elimu pekee, vijana wanaweza kubadilishwa kuwa wataalam watakaoisaidia nchi hii kuimarisha uchumi wake unaoendelea kuzorota.

Awali akiwahutubia waumini katika kanisa hilo, waziri huyo mkuu wa zamani alitoa wito wa umoja kabla na baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Nchi zilizostawi zatakiwa kufadhili elimu katika mataifa maskini

Kupitia wito wake wa Azimio La Umoja,Raila aliwahimiza wakenya kukumbatiana na kufanya kazi kwa pamoja kama familia moja kwa minajili ya taifa.

Akiwa ameandamana na aliyekuwa spika wa bunge la kitaifa Francis Ole Kaparo na Gavana wa Laikipia Nderitu Muriithi, Raila aliwaraia wakazi wa Mlima Kenya kuunga mkono azma yake ya kuwania urais. Alisema kinyume na naibu Rais William Ruto, yeye ana mpango dhabiti kuhakikisha taifa hili haliungani tu, lakini pia inastawi.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi