Raila awashtumu wanaokosoa mpango wa BBI

Aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga amewasuta wale wanaopinga marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa, BBI, akikariri kwamba hakuna awezaye kusimamisha raggae.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa zoezi la kukusanya saini katika Ukumbi wa KICC, Raila amewataja wale wanaodai kuwa BBI inalenga kulemaza mafanikio ya katiba ya 2010 kuwa manabii wa uongo.

Also Read
Viongozi wa kaunti ya Mombasa waelezea wasiwasi kuhusu kutoweka kwa watu

Raila amesema nchi hii imeanza safari ya kushughulikia maswala muhimu ambayo yamebaki kuwa changamoto nchini, na safari hiyo haiwezi kusimamishwa.

Kiongozi huyo wa chama cha ODM ametumia fursa hiyo kutetea baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti ya BBI.

Also Read
Tume ya IEBC yapinga mapendekezo ya BBI

Amesema pendekezo la kuundwa kwa afisi ya kupokea malalamishi ya umma kuhusu Idara ya Mahakam ani hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba idara hiyo inafanyiwa uangalizi.

Akirejelea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002, Raila amesema lilikuwa zoezi lenye uwazi zaidi baada ya vyama vya kisiasa kuhusika katika uteuzi wa makamishna wa kusimamia uchaguzi, kama inavyopendekezwa na ripoti ya BBI kuhusu uteuzi wa makamishna wa IEBC.

Also Read
Ukusanyaji saini za BBI kuanza rasmi leo

Raila amewahimiza Wakenya kujitokeza kwa wingi kuweka sahihi zao kwenye fomu za BBI zitakazozungushwa kote nchini na hatimaye kuunga mkono mswaada wa marekebisho ya katiba wa mwaka wa 2020 utakaofuata.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi