Raila hategemei kuidhinishwa na Uhuru ili kugombea urais, wasema baadhi ya viongozi wa ODM

Baadhi ya viongozi wa chama cha ODM wamesema si lazima Rais Uhuru Kenyatta amwidhinishe Raila Odinga kuwa mgombeaji wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Viongozi hao wamesema Raila hategemei kuidhinishwa na Rais Kenyatta bali anatilia maanani kupitishwa kwa mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa BBI.

Also Read
Jenerali Kibochi: Jeshi lina jukumu la kuisaida serikali katika nyanja zote

Wamesema hayo wakati wa mechi ya gofu ya kuadhimisha miaka 27 ya ukumbusho wa Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu.

Raila hajatangaza wazi iwapo atagombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku chama hicho cha ODM kikiwa katika harakati ya kumtafut amgombea atakayepeperusha tiketi ya chama hicho..

Also Read
Balozi wa Marekani ashtumu hatua ya kutumia vijana kuzua vurugu humu nchini

Raila kwa upande wake amejiepusha na siasa za urithi na kusisitiza kuwa nchi hii haina viongozi waaminifu watakaotetea maslahi ya taifa hili.

Kwa mara nyengine Raila amemkosoa Naibu Rais William Ruto kwa kueneza kampeni ya kimatabaka akisema kampeni hiyo itakuwa na athari kubwa kwa uwiano wa taifa hili.

Also Read
Martin Wambora ndiye mwenyekiti mpya wa Baraza la magavana

Chama cha ODM kimetangaza nafasi kwa wale wanaotaka kuwania urais kwa tikiti ya chama hicho kutuma maombi yao.

Raila huenda akang’ang’ania tiketi ya chama hicho na naibu wake kwenye uongozi wa ODM, aliye pia Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi