Raila na Ruto sako kwa bako katika kinyang’anyiro cha Urais

Waaniaji Urais William Ruto na Raila Odinga wako bega kwa bega kwenye matokeo ya awalia ya Urais kutoka kwa takwimu za IEBC.

Hata hivyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Kenya tangu mfumo wa vyama vingi vya kisiasa idadi ndogo ya wapiga kura ilijitokeza wakiwa milioni 12 065,803 kati ya milioni 22 nukta 1 ,waliojisali kuwa wapiga kura ikiwa takriban asilimia 57.

Also Read
Albert Wesonga ateuliwa meneja mpya wa AFC Leopards

Hii ina maana kuwa atakayetangazwa atakuwa Rais aliyechaguliwa na wachache.

Also Read
Raila akutana na waziri wa ulinzi wa Uingereza James Heappey

Matokeo ya awali yaashiria Ruto na Raila wakidhibiti ngome  zao ,Ruto akipata zaidi ya asilimia 80,  kutoka ngome yake kaskazini mwa bonde la ufa na,wakati Raila pia akipata asimilia 90 ya kura za Nyanza na eneo la mashariki na chini ya asilimia 20 kutoka Mlima Kenya.

Also Read
Raila amuidhinisha Abdulswamad Shariff Nassir kuwania ugavana wa Mombasa kwa tiketi ya ODM

Kulingana na hali ilivyo atakayeshinda kiti cha Urais itategemea uwezo wake wa kunyemelea ngome  za kura za mpinzani wake.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi