Raila Odinga anaongoza kwa umaarufu miongoni mwa wawaniaji Urais

Mgombeaji urais wa muungano wa Azimio la Umoja  Raila Odinga ndiye mgombea wa urais anayependelewa zaidi iwapo uchaguzi ungeandaliwa leo.

Kulingana na kura ya maoni iliyoandaliwa na kampuni ya Infotrak Research and Consulting, Raila anaongoza kwa asilimia  42 huku umaarufu wa mgombeaji urais wa muungano wa  Kenya Kwanza William Ruto ukiwa asilimia 38.

Also Read
Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Akiongea Jumanne asubuhi alipotangaza matokeo ya utafiti huo, afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya  Infotrak Angela Ambitho, alisema utafiti huo uliofanywa katika maeneo bunge yote 290, unaashiria kuwa  Raila angepata kura milioni  9.3 huku naibu rais  William Ruto akipata kura milioni  8.4.

Ambitho amesema hakuna kati ya wagombeaji hao wawili ambaye angepata kura 50 kuongeza moja ili aweze kutangazwa kuwa mshindi.

Also Read
Kamati ya bunge yapendekeza kupunguzwa kwa ushuru wa bidhaa muhimu

Ambitho alidokeza kuwa kaunti 11 za Pwani, Rift Valley, Kaskazini na Magharibi zitakuwa muhimu sana katika kuamua ni nani atakuwa Rais wa tano wa taifa hili.

Kaunti za Magharibi ni Bungoma na Transnzoia, kaunti za Rift Valley ya Kaskazini ni Samburu, Nakuru na Pokot Magharibi huku kaunti za RiftValley ya Kusini zikiwa  Narok na Kajiado.

Also Read
Makala ya 22 ya michezo ya jumuiya ya madola yafunguliwa rasmi Birmingham

Kaunti za Pwani ni pamoja na  Kwale, Lamu na Tana River.

Utafiti huo unaashiria kuwa  Raila angeongoza katika kaunti 20 huku  Ruto akiongoza katika kaunti 16 .

Jumla ya watu  9,000 walihojiwa kati ya tarehe 23 na 27 mwezi Mei katika kaunti zote 47.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi