Mgombeaji urais wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, ametangaza sehemu ya baraza lake la mawaziri kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa tarehe tisa mwezi Agosti mwaka 2022.
Kulingana na Raila, aliyekuwa spika wa bunge la kitaifa Kenneth Marende, sasa atakuwa spika wa bunge la Seneti huku gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ambaye muhula wake umekamilika akiwa waziri wa fedha.
Peter Munya atadumisha wadhifa anaoshikiliwa kwa sasa wa waziri wa kilimo lakini atakuwa na majukumu zaidi ya kuwa msimamizi wa sekta ya uzalishaji.
Gavana wa Mombasa anayeondoka Ali Hassan Joho atakuwa waziri wa ardhi na miongoni mwa majukumu yake ni kushughulikia dhuluma za jadi za ardhi katika eneo la pwani na kote nchini.
Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka amepatiwa wadhifa wa msimamizi wa baraza la mawaziri, licha ya kwamba tayari ametangaza kuwa atawania wadhifa wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Martha Karua atakuwa naibu rais na waziri wa haki na masuala ya kikatiba,