Raila Odinga: Mimi ni mcha Mungu

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amepuuzilia mbali madai kwamba hamwamini Mungu huku akitoa ushahidi kuhusu matukio ya maisha yake aliyosema yanatokana na baraka za Mwenyezi Mungu.

Waziri huyo mkuu wa zamani alielezea matukio yaliyoikumba familia yake,magumu aliyopitia kisiasa, mauaji ya marafiki wake na mateso aliyoyapata akiwa gerezani.

“Ni nani ambaye hawezi mwamini Mungu hasaa baada ya yale ambayo nimepitia pamoja na familia yangu? Nimeshuhudia wanaume na wanawake tuliokuwa nao wakiuawa, wengine wakipotea bila kupatikana huku wengine wakiteswa hadi kufariki…Ni kwa neema ya Mungu kwamba nilinusurika hayo yote….nina mwamini Mungu,”alisema Raila.

Kiongozi huyo wa upinzani aliwahimiza viongozi wa kidini kutoruhusu makanisa kutumiwa vibaya na wanasiasa.

Aidha Odinga aliwahimiza viongozi hao wasikubali kupokea pesa kutoka kwa wanasiasa bila kujua zilikotoka pesa hizo.

Kulingana na kinara huyo wa ODM, kufaya hivyo huenda kukayatumbukiza makanisa kwenye njama ya ulanguzi wa kifedha.

“Tunaunga mkono ukuaji wa kanisa….tunaunga mkono ufadhili wa kanisa lakini tunapinga kutumia kanisa kuendesha siasa. Watu pia hawapaswi kutumia kanisa katika ulanguzi wa pesa,”alisema Raila.

 

Also Read
UDA yakaribisha maombi kwa wanaotaka kuwania nyadhifa tatu za MCA
Also Read
Watu 15 wakamatwa kwa kukiuka sheria za usafiri wa majini

Akiongea kwenye mkutano na viongozi wa kidini katika jumba la Ufungamano, Raila aliwarai kuunga mkono mchakato wa BBI akisema utawafaidi wakenya.

Raila alisema ripoti ya BBI itahakikisha usawa katika ugavi wa mapato huku akipuuzilia mbali mdahalo kuhusu matabaka unaendelea humu nchini akisema taifa hili haliwezi kusonga mbele ikiwa dhana kuhusu wenye mali na wasio na mali itaendelezwa.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi