Rais Kenyatta aanza ziara nchini Ushelisheli

Rais Uhuru Kenyatta leo ameanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Ushelisheli.

Wakati wa ziara hiyo , rais Kenyatta ataandaa mazungumzo ya pande mbili na rais Wavel Ramkalawan wa nchi hiyo kabla ya kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba mbali mbali inayoangazia juhudi za kuimarisha uhusiano wa kijamii na kiuchumi na kitamaduni kati ya nchi hizi mbili.

Also Read
Ruto asema ataboresha uchumi wa Pwani akichaguliwa Rais


Rais Kenyatta pia amepangiwa kuhutubia kikao kisicho cha kawaida cha bunge la kitaifa la Ushelisheli mbali na mikutano mingine ya kujadili maslahi ya nchi hizi mbili.

Also Read
Rais Kenyatta awarai wawekazi wa Ufaransa kuchagua Kenya kwa uwekezaji wao

Kenya na Ushelisheli zinashirikiana katika nyanja mbali mbali ikiwemo biashara , usalama wa baharini na vita dhidi ya uharamia , uchimi wa shughuli za majini , ushirikiano wa vyama vya wafanyabiashara , vijana na michezo, utamaduni na uvuvi miongoni mwa nyanja nyingine.

Also Read
Rais Kenyatta apongeza mafanikio dhidi ya uwindaji haramu

Hiyo ni ziara ya kwanza ya kiserikali ya rais Kenyatta nchini Ushelisheli.

  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi