Rais Kenyatta afadhaishwa na ongezeko la dhuluma za kijinsia Afrika

Rais Uhuru Kenyatta amefadhaishwa na ongezeko la visa vya dhuluma za kijinsia barani Afrika akisema hali hiyo imefikia viwango vya kuogofya.

Rais amesema ugonjwa wa COVID-19 umezidisha hali hiyo na kutoa kuwe na hatua za dharura za kimataifa kukomesha visa hivyo.

Also Read
WHO yaanzisha uhamasisho kuhusu aina mpya ya Corona Uingereza

Rais Kenyatta amesema serikali itawekeza dola milioni 23 katika mipango ya kukomesha dhuluma za kijinsia ifikapo mwaka ujao na kuongeza kiasi hicho hadi dola milioni 50 kufikia mwaka 2026.

Also Read
Rais Kenyatta amuomboleza Seneta wa Garissa Yusuf Haji

Fedha hizo ni pamoja na dola milioni moja kila mwaka zitakazotengewa utafiti na kuwakimu wahanga wa dhuluma za kijinsia.

Also Read
Watu 528 waambukizwa Covid-19 nchini huku watu wanne wakifariki

Rais alisema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kuhusu usawa wa kizazi mjini Paris, Ufaransa.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi