Rais Kenyatta ahudhuria mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Juja Francis Waititu

Rais Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa wageni mashuhuri ambao wanahudhuria ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu, maarufu kama ‘Wakapee’.

Ibada hiyo, ambayo imeng’oa nanga mwendo wa saa nne asubuhi, inaandaliwa katika uwanja wa kufuzia wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia (JKUAT).

Also Read
Visa 138 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa humu nchini

Itakapotamatika ibada hiyo, mwili wa mwendazake mbunge huyo utasitiriwa nyumbani kwake katika eneo la Juja, Kaunti ya Kiambu.

Also Read
Mudavadi amtaka Ruto awe na msimamo kuhusu BBI

Waititu aliaga dunia wiki jana kutokana na ugonjwa wa saratani ya ubongo aliopigana nao tangu mwaka wa 2017.

Also Read
Wakazi wa Mbeere kunufaika na mradi wa shilingi milioni 220 wa unyunyiziaji maji

Mbunge huyo alitajwa kama kiongozi wa maenedeleo, aliyejitolea na ambaye matendo yake yaliambatana na mahitaji ya wananchi aliowakilisha bungeni.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi