Rais Kenyatta akutana na mwenzake wa Ufaransa mjini Paris

Rais Uhuru Kenyatta leo amekutana na mwenyeji wake wa Ufaransa, Emmanuel Macron katika makao ya Elysee mjini Paris ambako viongozi hao wawili walijadili masuala kadhaa yenye manufaa kati ya nchi hizi mbili.

Rais Kenyatta na mwenzake wake wa Ufaransa walijadili ufanisi wa miradi ya miundo msingi inayofadhiliwa na Ufaransa humu nchini, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa barabara ya kilomita 233 kutoka Rironi kupitia Nakuru hadi Mau Summit, ambayo ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Septemba mwaka huu.

Also Read
Watu 36 waorodheshwa kwa wadhifa wa makamishna wa IEBC

Makubaliano kati ya sekta za umma na kibinafsi ya kupanua barabara inayoelekea Kaskazini mwa nchi kuwa ya safu nne pande mbili ili kupunguza msongamano wa magari kwa gharama ya shilingi bilioni 160 yaliafikiwa wakati wa ziara ya Rais Kenyatta nchini Ufaransa mwezi Oktoba mwaka jana.

Also Read
Rais Kenyatta amuomboleza Askofu Morris Mwarandu

Mbali na miundo msingi, marais Kenyatta na Macron walijadili kuimarishwa ushirikiano katika sekta ya afya, hasa katika kukuza uwezo wa nchi hii wa kutengeneza chanjo.

Kuhusu masuala ya kimataifa, viongozi hao wawili walishauriana kuhusu kongamano lijalo mjini London la ushirikiano wa kimataifa kuhusu sekta ya elimu, ambalo wenyeji wenza wake watakuwa Rais Kenyatta na Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson.

Also Read
Nchi za ulaya zatakiwa kutoa asilimia tano ya chanjo ya Covid-19 kwa nchi zinazostawi

Kongamano hilo linatarajiwa kuandaliwa kati ya tarehe 28 na 29 mwezi huu na linalenga kukusanya dola bilioni 5 katika muda wa miaka mitano kwa uwekezaji katika elimu ya watoto milioni 175 kwenye nchi zenye mapato ya chini kote duniani.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi