Rais Kenyatta akutana na Waziri kutoka Japan katika Ikulu ya Nairobi

Rais Uhuru Kenyatta amekutana na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Japan anayezuru humu nchini, Toshimitsu Motegi, katika Ikulu ya Nairobi.

Wakati wa mkutano huo, Motegi, ambaye yuko kwenye ziara ya siku mbili humu nchini, ameeleza kuendelea kujitolea kwa Japan kuunga mkono mipango ya maendeleo humu nchini, hasa miradi ya muundo msingi.

Also Read
Rais Kenyatta amteua Jamleck Muturi kuwa mwenyekiti wa TSC

Motegi ametaja mradi unaoendelea wa kupanua Bandari ya Mombasa na ustawishaji eneo maalum la kiuchumi la Dongo Kundu kuwa baadhi ya miradi ambayo serikali yake inamakinika kuhakikisha imekamilishwa.

Also Read
Kenya yanakili visa 1,279 vipya vya Covid-19

Waziri huyo wa Japan pia amemuarifu Rais Kenyatta kuhusu kongamano la kibiashara kati ya Japan na Kenya ambalo litaandaliwa baadaye mwaka huu nchini Japan na akawasilisha mwaliko wa Waziri Mkuu Yoshide Suga kwake.

Also Read
Watu 18 zaidi wafariki hapa nchini kutokana na Covid-19

Kwa upande wake Rais Kenyatta ameeleza kutambua hatua ya Japan kuendelea kuunga mkono mipango ya maendeleo humu nchini, akisema nchi hii itaendelea kuimarisha uhusiano wake wa kihistoria na taifa hilo la Bara Asia.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi