Rais Kenyatta alenga kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Uingereza

Rais Uhuru Kenyatta alikutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, kwa mazungumzo ya pande mbili mnamo siku ya pili ya ziara yake rasmi  nchini Uingereza. 

Mkutano wa viongozi hao ulifanyika  katika makao rasmi ya Waziri Mkuu yalioko Checkers  huko Buckinghamshire na   walijadili kuhusu kuimarishwa  kwa uhusiano wa kihistoria  kati  ya  Kenya na Uingereza na pia kuangazia  njia mpya za kuimarisha  ushirikiano  kati ya nchi hizo mbili.

Katika mazungumzo yao mapana, Rais na Waziri Mkuu walikariri dhahiri  kwamba ilikuwa muhimu kuimarisha manufaa ya ushirikiano wa kimkakati waliotia saini  kwenye  ziara ya awali ya   Rais  Uhuru Kenyatta nchini  Uingereza.

Rais alisema utekelezaji wa  maafikiano hayo uliathiriwa na janga la  Covid-19 lakini nchi hizo mbili lazima sasa zianze kutekeleza makubaliano hayo.

Rais Uhuru Kenyatta akutana na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Johnson alisisitiza kujitolea kwa utawala wake kuendelea kufanya kazi na Kenya katika kupanua biashara za Uingereza barani Afrika ili kuzuia  kupungua kwa uwekezaji wa Uingereza katika bara hili.

Waziri Mkuu Johnson aliahidi   nyongeza  ya chanjo  kwa  Kenya  ya  zaidi ya  dozi  alfu 400 zilizotangazwa  awali.

Viongozi hao wawili pia wamejadili maswala  kadhaa yanayohusu  mataifa yao  ikiwa ni pamoja na amani na usalama wa   kanda hii.

Rais Kenyatta aliandamana na mawaziri Ukur Yatani wa fedha, Raychelle Omamo wa maswala ya nchi za kigeni na Dkt Monicah Juma wa ulinzi.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi