Rais Kenyatta amuomboleza Askofu Morris Mwarandu

Rais Uhuru Kenyatta amepeleka risala za rambi rambi kufuatia kifo cha Askofu Morris Mwarandu, mwanzilishi wa kanisa la “The Lord’s Gathering Fellowship Church.”

Rais Kenyatta amemtaja Askofu Mwarandu kuwa mkristo halisi ambaye alijitolea kukuza imani, nyoyo na pia nguvu za watu wote.

Askofu Mwarandu, ambaye alikuwa na umri wa miaka 73, alifariki Jumamosi usiku katika hospital moja ya Nairobi ambako alikuwa akipokea matibabu.

Katika risala zake kwa familia, jamaa na pia waumini wote wa kanisa la “The Lord’s Gathering Fellowship Church”, Rais Kenyatta alisema inasikitisha kuona kwamba kifo kimetupokonya mtumishi halisi wa mwenyezi mungu wakati ambapo watu wengi wanamtegemea kwa chakula cha kiroho.

Alisema Askofu Mwarandu atakumbukwa kama Muinjilisti hodari ambaye nyakati zote aliona wema hata katika mazingira magumu.

Rais Kenyatta alimuomba Mwenyezi Mungu kumpnguvu na faraja Mama Christine Ega Mwarandu, Familia na pia waumini wote wa kanisa la “The Lord’s Gathering Fellowship Church”,wanapoomboleza kifo cha Askofu huyo.

Naibu Rais William Ruto pia amemwomboleza Askofu Mwarandu kama mtumishi aliyejitolea kuhudumia kanisa na pia Mungu, na kuwaombea faraja familia na marafiki wa Askofu huyo.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi