Rais Kenyatta amuomboleza mfanyibiashara Ahmed Abdulle

Rais Uhuru  Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kwa familia, jamaa na marafiki wa mwanzilishi  wa kampuni ya Dakawou Transporters, Haji Ahmed Nuur Abdulle aliyefariki siku ya Jumamosi.

Katika ujumbe wake wa faraja, kiongozi wa taifa alimwomboleza Abdulle aliyekuwa na umri wa miaka 69, akimtaja mwanabiashara shupavu aliyeanzisha na kuongoza kwa ufanisi kampuni ya usafirishaji gesi ya  Dakawou Transporters.

Also Read
Shujaa yatitigwa na Fiji 29-5 msururu wa Tolouse

Rais alidokeza kuwa, kupitia kwa kampuni ya Dakawou Transporters na biashara zingine,  marehemu Abdulle alitoa nafasi za kazi kwa maelfu ya wakenya.

“Abdulle alikuwa mnyenyekevu na mfanyibiashara mwenye bidii aliyechangia pakubwa kwa ukuaji wa uchumi kwa kubuni nafasi za biashara kwa watu wetu na nafasi za kazi kwa vijana wetu kupitia kampuni hiyo pamoja na biashara zingine,”alisema Rais.

Also Read
Familia milioni 1.2 kunufaika na mpango wa huduma nafuu za afya

” Hata tunapoomboleza kifo chake, tunashukuru Mungu kwa maisha yake ya ufanisi, hasaa katika tasnia ya biashara ambapo alichangia pakubwa ukuaji wa uchumi wa taifa hili,” aliomboleza Rais.

Also Read
Maafisa wa polisi waonywa dhidi ya utovu wa nidhamu

Kando na biashara, marehemu Abdulle alishirikiana na wengine kujenga taasisi za elimu na kidini katika kaunti ya Mombasa na katika sehemu zingine za nchi.

Rais alimwomba Mwenyezi Mungu kuipa familia hiyo nguvu wakati huu mgumu wa kuomboleza.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi