Rais Kenyatta amwomboleza Khalid Hossain Ahmed ambaye ni mume wa waziri Amina Mohamed

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambirambi kwa familia ya waziri wa michezo Amina Mohamed kufuatia kifo cha mumewe Khalid Hossain Ahmed.

Ahmed, ambaye ni mfanyibiashara Jijini Nairobi, aliaga dunia Alhamisi asubuhi alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Jijini Nairobi.

Katika ujumbe wake wa faraja kwa familia, jamaa na marafiki wa waziri huyo, Rais Kenyatta alimuomboleza Ahmed akimtaja mtu muungwana na aliyekuwa nguzo muhimu katika familia yake.

Ahmed alikuwa mjasiri na nguzo muhimu katika familia yake. Natuma rambirambi zangu kwa mfanyikazi mwenzangu Amina, watoto na familia kutokana na kifo cha bwana Ahmed,” aliomboleza Rais.

Kiongozi wa taifa ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Uingereza, alimkumbuka mwendazake kuwa mfanyibashara shupavu.

Ni jambo la kusikitisha kuwa kifo kimetupokonya mwanabiashara shupavu ambaye mchango wake katika maendeleo ya taifa hili utakoswa,” alisema Rais.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Mzozo wa kidiplomasia kati ya Uchina na nchi za magharibi wasitishwa

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi