Rais Kenyatta aomboleza kifo cha shujaa wa raga Benjamin Ayimba

Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kwa jamaa, familia na marafiki wa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande, Benjamin Ayimba.

Ayimba, aliyekuwa na umri wa miaka 44, alifariki Ijumaa usiku katika hospitali moja jijini Nairobi ambako amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa malaria inayoathiri ubongo kwa mwezi mmoja uliopita.

Rais Kenyatta amemtaja Ayimba kama Mkenya shupavu na mwanaspoti hodari aliyehimiza kizazi kipya cha Wakenya kujiunga na mchezo wa raga.

Also Read
Rais Kenyatta aongoza hafla ya ufunguzi wa Kichinjio cha kisasa cha Neema

Rais alisema Ayimba aliandikisha matokeo bora katika mchezo wa raga hususan mnamo mwaka wa 2016 wakati Kenya, chini ya ukufunzi wake, ilishinda taji ya dunia ya mchezo wa raga wa wachezaji saba kila upande nchini Singapore baada ya kuwabwaga Fiji.

Rais alisema Ayimba aliinua hadhi ya mchezo wa raga humu nchini kufikia viwango vya kimataifa ambapo Kenya ilitambuliwa miongoni mwa mataifa ibuka kwenye raga ya wachezaji saba kila upande.

Rais alimuomba Maulana kuipa faraja familia yake wanapoomboleza kifo cha shujaa huyo.

Also Read
Wafanyikazi 9,144 walio mstari wa mbele wamechanjwa dhidi ya Covid-19 hapa nchini

Aidha, Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa viongozi waliotuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha Ayimba.

Kwenye ukurasa wa twitter, Ruto alimtaja marehemu Ayimba kama nyota na mmoja wa wanamichezo mashuhuri ulimwenguni.

Alisema Ayimba alikuwa mchezaji raga mashuhuri na kocha aliyekuwa na ari kubwa ya kuafikia malengo yake.

Also Read
Kenya yajiunga na ulimwenguni kuadhimisha siku ya Malaria Duniani

Ruto alisema Wakenya watakumbuka daima ukakamavu na mafanikio yake kwenye mchezo wa raga humu nchini.

Na kwenye ukurasa wake wa facebook, Odinga alimtaja marehemu Ayimba kama mzalendo aliyeliletea taifa hili sifa sufufu kupitia mchezo wa raga, huku akitaja ushindi wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande wakati wa mashindano ya mwaka 2016.

Kwa upande wake Kalonzo alisema kifo cha Ayimba ni pigo kwa jamii ya wachezaji raga humu nchini.

  

Latest posts

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi