Rais Kenyatta aongoza hafla ya ufunguzi wa Kichinjio cha kisasa cha Neema

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza hafla ya ufunguzi rasmi wa kichinjio cha kisasa cha Neema katika eneo la Lucky Summer, Kaunti ya Nairobi.

Taarifa kutoka Ikulu ya Rais imesema kuwa kichinjo hicho kinatayarisha aina mbali mbali za bidhaa za nyama kwa soko la humu nchini na kuuzwa nje.

Also Read
Watu 7 zaidi wafariki kutokana na makali ya Covid-19 hapa nchini

Kichinjio hicho kinamilikiwa na wafugaji wa humu nchini na kina uwezo wa kuchinja mbuzi na kondoo kati ya 1,200 na elfu sita.

Haya yanajiri siku chache baada ya Rais Kenyatta kufungua tena kiwanda cha utayarishaji nyama cha KMC kilichokarabatiwa huko Athi River, Kaunti ya Machakos siku ya Jumatatu.

Wakati wa hafla hiyo Rais Kenyatta alisema kuwa lengo la serikali ni kuimarisha sekta ya ufugaji kuwa kitovu kikuu cha kiuchumi.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi