Rais Kenyatta apongeza ujenzi unaoendelea wa barabara ya moja kwa moja

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi, alifanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya moja kwa moja ya kilomita 27.1 jijini Nairobi ambapo alieleza kuridhika kwake na kazi inayotekelezwa katika barabara hiyo muhimu.

Itakapokamilika mwezi Machi mwaka 2022, barabara hiyo yenye safu nane inatarajiwa kupunguza vilivyo msongamano wa magari katika barabara ya Mombasa na kupunguza muda wa usafiri kati ya Mlolongo na Westlands kwa dakika 20.

Also Read
Serikali kusuluhisha tatizo la jadi kuhusu ardhi kupitia utoaji hatimiliki

Wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi, rais Kenyatta, ambaye aliandamana na waziri wa muundo msingi James Macharia na mkurugenzi wa shirika la huduma kwa jiji la Nairobi, Mohamed Badi, aliweka jiwe la msingi kwa daraja la mwisho, baada ya jiwe la kwanza la msingi kuwekwa tarehe 26 mwezi Disemba mwaka wa 2020.

Also Read
Rais Kenyatta na Suluhu waahidi kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya Kenya na Tanzania

Kiongozi wa nchi alimpongeza mwanakandarasi wa mradi huo kwa kazi nzuri na kuelezea imani kwamba barabara hiyo itakuwa tayari kwa matumizi mwezi Machi mwaka ujao.

Akisema barabara hiyo imejengwa chini ya ushirikiano wa sekta za umma na kibinafsi, rais Kenyatta alikariri kujitolea kwa nchi hii kuendelea kushirikiana na serikali ya China ambayo alisema inaendelea kuwa mshirika mkuu wa kimaendeleo wa nchi hii.

Also Read
Onyango kutetea mkanda wa Welter dhidi ya Nyakesha Disemba 4

Alisema barabara hiyo ya moja kwa moja imebuni zaidi ya nafasi elfu-6 za ajira, kuwanufaisha wenye kandarasi ndogo 200 na mamia ya wauzaji bidhaa za ujenzi wa humu nchini.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi