Rais Kenyatta atia saini mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya kisiasa

Siku moja baada ya bunge la Senate kupitisha mswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya kisiasa, Rais Uhuru Kenyatta ametia saini mswada uliopitishwa hivi majuzi wa marekebishon ya sheria ya vyama vya kisiasa kuwa sheria.

Mswada huo ulipitishwa na bunge la kitaifa wakati wa msimu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya kabla ya kuwasilishwa kwa bunge la Senate ambalo lilipitisha Jumatano wiki hii.

Also Read
Uchukuzi wa gari moshi katika Jiji la Nairobi kurejelewa Jumatatu

Sheria hiyo mpya inafanyia marekebisho sheria ya vyama vya kisiasa ya mwaka 2011 kwa kuanzisha vyama vya kisiasa vya miungano, kufafanua shughuli za vyama vya kisiasa na vile vile kubadilisha utaratibu na masharfti ya kufuzu kwa vyama vya kisiasa kupokea pesa kutoka kwa hazina ya kufadhili vyama vya kisiasa.

Sheria hiyo pia inawezesha msajili wa vyama vya kisiasa kuratibu orodha za wanachama wa vyama pamoja na sheria za uchaguzi wa mchujo wa vyama kwa lengo la kuimarisha usimamiz wa vyama vya kisiasa na kudumisha demokrasia nchini.

Also Read
Wanaounga mkono BBI wana muda hadi Jumatatu kudhibitisha maelezo yao

Mswada huo uliwasilishwa kwa Rais kuutia saini wakati wa hafla fupi katika ikulu ya Nairobi iliyohudhuriwa na mkuu wa utumishi wa umma Dkt. Joseph Kinyua, Spika wa seneti Keneth Lusaka,spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi pamoja na kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Samuel Poghisio na mwenzake katika bunge la kitaifa Amos Kimunya.

Also Read
Rais Kenyatta awasili Ukambani kukagua Miradi ya maendelo

Sheria hiyo ilisababisha malumbano makali kati ya mrengo unaomuunga mkono naibu Rais William Ruto na mwingine ukiunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

 

  

Latest posts

Kenya imenakili visa 26 vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Rais Kenyatta: Mataifa ya Afrika Sharti yakabiliane kikamilifu na zimwi la Ufisadi

Tom Mathinji

Wanamichezo 11 wapokea msaada wa masomo kutoka kwa kamati ya Olimpiki nchini NOCK

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi