Rais Kenyatta atoa wito wa kuharakishwa kwa sheria ya matibabu kwa wote

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito wa kuharakishwa kupitishwa kwa sheria inayonuiwa kuhakikisha bima ya matibabu kwa wote.

Akizungumza Alhamisi asubuhi, wakati wa mkutano wa maombi kwa taifa katika majengo ya Bunge, Rais Kenyatta aliwataka wadau wote kuharakisha utekelezwaji wa mapendekezo yaliyotolewa kuhakikisha wakenya wote wana bima ya matibabu ili kila mkenya aweze kupata matibabu ya bei nafuu hasa wakati huu wa kipindi cha tandavu ya covid-19.

Aidha Rais alikariri wito wake kwa viongozi na wakenya kwa ujumla kudumisha Amani kwa manufaa ya ufanisi wa taifa.

Kwa upande wake naibu Rais William Ruto, aliomba kuwepo kwa mazungumzo katika juhudi za kutatua mitazamo tofauti kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kama vile mapendekezo ya marekebisho ya katiba.

Also Read
Mahakama ‘yaidhinisha’ mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Matungu Justus Murunga

Aliyekuwa mkuu wa sheria Amos Wako amehimiza WaKenya wawe wakienda kupimwa ugonjwa wa Covid-19 mara tu wanapohisi dalili za ugonjwa huo.

Seneta huyo wa kaunti ya Busia alisema yeye mwenyewe nusra apoteze maisha yake alipo-ambukizwa virusi vya ugonjwa huo kwa sababu alipuuza baadhi ya dalili kama zile za matatizo ya kupumua na kisulisuli.

Wako ambaye alipatwa na ugonjwa wa Covid-19 mwezi Februari mwaka huu, anasema kuchelewa kutibiwa kulifanya hali yake kuwa mbaya zaidi.

Also Read
Wakenya watakiwa kuwaheshimu viongozi na kudumisha amani

Alishauri wakenya kuto-puuza ishara zozote, na pia waache kujinunulia madawa, akisema huenda wakafanya hali zao kuwa mbaya zaidi, badala ya kutibiwa kwa urahisi.

Aidha, Wako aliitaka serikal kuongeza juhudi zake mara dufu katika kufanikisha mpango wa afya kwa wote, akisema kuna wakenya wengi ambao bado hawamudu gharama za matibabu.

Aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu Edward Ouko leo alielezea changamoto alizozipata alipokuwa akitekeleza majukumu yake katika wadhifa huo.

Akiongea kwa njia ya video wakati wa mkutano wa 18 wa maombi ya kitaifa, Ouko alisema kuwa uongozi hukumbwa na changamoto si haba hasa wale walio kwenye nyadhifa ambapo maamuzi yasiyopendelewa na wengi yanatolewa.

Also Read
Biashara za mtandaoni kutozwa ushuru

Alisema aliamua kuwa akiomba kila mara aliposhtumiwa na watu ambao hawakufurahishwa na ripoti zake za ukaguzi wa hesabu.

Alisema kuwa viongozi ni sharti wawe tayari kupingwa hali ambayo hujitokeza katika madai ambayo hayabainishwi aliyeyatoa ambayo mara nyingi hufichuliwa kwa vyombo vya habari.

Ouko alizungumzia hali ambapo rufaa iliwasilishwa kumwondoa wadhifani akisema inasikitisha kuwa baadhi ya madai yalicyochewa na wafanyikazi wa afisi alikohudumu.

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi