Rais Kenyatta awaalika hapa nchini wawekezaji kutoka Milki za Kiarabu

Na Ripota wetu.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye yuko katika ziara rasmi katika muungano wa Milki za Kiarabu, amehakikishia mataifa ya eneo la guba kuwa serikali yake itazindua mazingira muafaka ya biashara nchini ili kuwawezesha wafanyibiashara kutoka mataifa hiyo kuwekeza katika soko la Afrika.

Also Read
Kenya na Tanzania zajitolea kuboresha uhusiano baina yazo

Akiongea wakati wa kikao cha kibiashara baina ya Kenya na mataifa ya guba  nchini Dubai, Rais Kenyatta aliwaalika hapa nchini wawekezaji katika sekta kama vile kilimo,kawi,teknolojia ya habari na uchumi wa shughuli za majini.

Rais Kenyatta akutana na wawekezaji kutoka eneo la ghuba.

Akiongea rais wa shirika la wenye biashara na viwanda nchini chama Richard Ngatia alikariri umuhimu wa Kenya kama kiingilio cha soko la Afrika.

Also Read
Rais Kenyatta ampongeza Emmanuel Macron kwa kuchaguliwa tena kuongoza Ufaransa

Aliyahimiza mataifa ya guba kuwekeza humu nchini akiongeza kwamba bandari ya Mombasa ni kitovu muhimu cha uchukuzi katika kanda hii inayojumuisha Uganda, Sudan kusini , Rwanda na Burundi.

Also Read
Rais Kenyatta aondoa makataa ya kuto-toka nje wakati wa usiku

Aliongeza kuwa mradi wa Lapsset uatakapokamilika, utaimarisha shughuli za uchukuzi baina ya Kenya na mataifa ya Sudan kusini, Ethiopia na Uganda na pia kuimarisha biashara baina ya mataifa ya guba na yale ya kusini mwa Afrika.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi