Rais Kenyatta awapongeza wafanyikazi wa ikulu

Rais Uhuru Kenyatta amewapongeza wafanyikazi wa Ikulu kwa kujitolea kulitumikia taifa hili.

Rais Kenyatta aliwashukuru kwa jukumu walilotekeleza katika kumsaidia kutimiza majukumu yake akiwa kiongozi wa taifa.

“Kwa niaba yangu na ya Mama Taifa na familia nzima kwa Jumla, tunafuraha kwa nyinyi wote, idara zote za Ikulu, kwa kuwa tumefanya kazi kwa ushirikiano. Tutawakosa sana lakini tutakuwa na kumbukumbu jinsi tulivyofanya kazi pamoja,” alisema Rais.

Also Read
Australia kuwatumia wanajeshi kutekeleza masharti dhidi ya Covid-19

Kiongozi wa taifa alisema hayo katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumapili, baada ya kuhudhuria ibada ya maombi ya shukrani na kuabudu kuadhimisha miaka 10 ya ufanisi wa rais na Mama wa Taifa Margaret Kenyatta.

Maombi hayo ya madhehebu mbalimbali yalihudhuriwa na wafanyikazi wa Ikulu zote pamoja na Ikulu ndogo wakiongozwa na msimamizi wa Ikulu Bw. Kinuthia Mbugua na msimamizi wa wafanyikazi katika afisi ya mama wa taifa Bi. Constance Gakonyo.

Also Read
Gharama ya umeme yapunguzwa hapa nchini

Rais Kenyatta aliwahimiza watakaosalia katika ikulu kuunga mkono serikali ijayo na kufanya kazi kwa bidii ili kulikuza taifa hili kimaendeleo.

“Jinsi tulivyowapata wengi wenu hapa, tutawaacha wengi hapa. Langu nikuwashauri kuunga mkono utawala unaokuja. Wasaidie kupiga hatua ili taifa letu lisonge mbele,” alishauri Rais Kenyatta.

Also Read
Visa vipya 1,205 vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Katika mahubiri yake, askofu wa kanisa la AIC hapa nchini, Abraham Mulwa alimpongeza rais Kenyatta kwa kujitolea kwake kutumikia taifa hili.

Maafisa wa serikali waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na waziri Margaret Kobia na Mkurugenzi Mkuu wa huduma za Jiji la Nairobi Mohamed Badi miongoni mwa wengine.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi