Rais Uhuru Kenyatta amewasili Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kuhudhuria kikao cha 35 cha kongamano la viongozi wa mataifa wanachama wa Muungano wa Afrika, ambacho ni cha kwanza kuandaliwa ana kwa ana tangu kuzuka kwa virusi vya Covid-19 mwaka 2020.
Katika mutano huo wa siku mbili, Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuwasilisha ripoti kuhusu mafanikio ya juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa Malaria, ripoti ya ajenda ya mwaka huu kuhusu amani na usalama pamoja na ajenda ya baraza la usalama.

Kiongozi wa taifa pia atahudhuria hafla ambapo atashuhudia Rais Macky Sall wa Senegal akichukua wadhifa wa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika kutoka kwa mwenyekiti wa sasa Rais Felix Tshisekedi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.