Rais Kenyatta awateua watu watano kujiunga na TSC

Rais  Uhuru Kenyatta amewasilisha majina ya watu watano  bungeni ili kuidhinishwa kuwa wanachama wa tume ya kuwaajiri walimu TSC.

Rais amewapendekeza  Dkt. Nicodemus Ojuma Anyang, Christine K. Kahindi, Sharon Jelagat Kisire, Annceta G. Wafukho na  Salesa Adano Abudo, kuteuliwa kuwa wanachama wa tume hiyo ya TSC.

Also Read
Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock wakamatwa na kupelekwa mafichoni

Majina yao yalikuwa kwenye arifa  iliyosomwa bungeni Alhamisi alasiri na spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi. Kwenye ujumbe wake Rais aliomba bunge kuyaweka kipaumbele majina hayo.

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi aliwasilisha majina hayo kwa kamati ya bunge kuhusu elimu inayoongozwa na mbunge Busia Florence Mutua.

Also Read
Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Huku bunge la kitaifa likitarajiwa kwenda likizoni tarehe 20 mwezi huu , rais ameomba bunge kuwafahamisha wateuliwa na umma kwa jumla kuhusu wakati na mahali pa kuandalia vikao vya kusikiliza suala hilo.

Also Read
Eugene Wamalwa amkabidhi rasmi Charles Keter wizara ya Ugatuzi

Baada ya kukamilika kwa vikao hivyo na kuidhinishwa kwa ripoti , basi  ripoti hiyo iwasilishwe bungeni ili bunge liweze kuijadili  katika kipindi cha siku 21.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi