Rais Kenyatta awateuwa Mabalozi na Makamishna wakuu

Rais Uhuru Kenyatta amewapendekeza na kuwateua makamishna wakuu na mabalozi watakaoakilisha nchi hii katika nchi mbalimbali.

wale walioteuliwa kuwa makamishna wakuu ni pamoja na balozi John Tipis kuhudumu nchini Australia, Immaculate Wambua kuhudumu nchini Canada na Catherine Mwangi kuhudumu nchini Afrika kusini.

Also Read
Rais Kenyatta aongoza mazungumzo kati ya wajumbe wa Kenya na wa Somaliland

Balozi Martin Kimani ameteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa nchi hii katika umoja wa mataifa.

Balozi Jean Kamau ameteuliwa kuwa balozi nchini Ethiopia, Linday Kiptiness kuhudumu nchini Thailand, balozi Tom Amolo kuhudumu nchini ujerumani, Lemarron Kaanto nchini Brazil, balozi Daniel Wambura nchini Burundi na Stella Munyi nchini Zimbabwe.

Also Read
Rais kenyatta atoa wito kwa wakenya kuendelea kuliombea taifa hili

Wengine ni meja jenerali Samuel Nandwa kuhudumu nchini Sudan kusini, Meja jenerali Ngewa Mukala kuhudumu nchini Sudan, balozi Benson Ogutu kuhudumu nchini Urusi, Joshua Gatimu nchini Iran, balozi Tabu Irina nchini Japan na balozi Jean Kimani huko New York.

Also Read
Raphael Tuju amfokea Naibu Rais William Ruto

Rais pia aliwateua makamishna watatu wa zamani wa tume ya IEBC, Consolata Nkatha, Margaret Mwachanya na Dr Paul Kurgat kuwa manaibu wakuu wa kibalozi nchini Italia, Pakistan na Urusi mtawalia.

 

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi