Rais Kenyatta awatuza washindi wa medali za Olimpiki

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu amekutana na baadhi ya washindi wa medali za Olimpiki kwa timu ya Kenya katika ikulu ya Mombasa.

Rais Kenyata pia ametangaza kuwa washindi wote wa nishani za dhahabu watatuzwa shilingi milioni 1 kila mmoja na shilingie elfu 750 kwa walioshinda medali za fedha wakati walionyakua nishani za shaba wakitunukiwa shilingi nusu milioni kila mmoja.

Also Read
Bingwa wa Afrika Vanice Kerubo ashinda mita 400 kuruka viunzi Kip Keino Classic

Wanariadha waliohudhuria kikao hicho na Rais katika ikulu ya Mombasa ni Peres Jepchircir aliyeshinda dhahabu ya marathonmshindi wa dhahabu ya mita 800 Emannuel Korir na washindi wa fedha Ferguson Rotich katika mita 800 ,Brigid Kosgei katika marathon  medali ya fedha,Hellen Obiri katika mita 5000,Timothy Cheruiyot katika mita 1500 na  Benjamin Kigen aliyenyakua shaba ya mita  3000 kuruka viunzi na maji.

Also Read
Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi
Rais Kenyatta akipiga picha na washindi wa medali pamoja na Rais wa shirikisho la riadha duniani katika ikulu ya Mombasa

Rais pia ametangaza tuzo ya shilingi laki 2 kwa kila afisa wa timu ya Kenya kwa michezo ya Olimpiki na kwa wale wa Olimpiki ya walamavu.

Also Read
Wahabeshi wawika nyumbani katika makala ya 20 ya Great Ethiopian Run

Kenya ilizoa jumla ya medali 4 za dhahabu nne za fedha na mbili za shaba ikiibuka ya kwanza Afrika na ya 19 kwa jumla.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Rais wa shirikisho la riadha ulimwenguni Seb Coe.

 

 

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi