Rais Kenyatta azindua hospitali ya kisasa ya kijeshi kaunti ya Meru

Rais Uhuru Kenyatta siku ya Alhamisi alifungua hospitali ya kisasa ya kuwahudumia maafisa wa vikosi vya ulinzi hapa nchini, hatua hii ikiwa ni kuambatana na lengo la serikali la kuboresha maslahi ya maafisa wa usalama na utoaji huduma bora kwa wakenya.

Hospitali hiyo ya kisasa ya kijeshi katika kaunti ya Isiolo iliyo na vitanda 105, inatarajiwa kukidhi mahitaji ya kiafya ya wanajeshi, familia zao na maafisa wa zamani wa idara hiyo katika eneo la Mashariki likijumuisha kaunti za Isiolo, Marsabit, Mandera, Wajir, Meru, Nanyuki na Samburu.

Also Read
Rais Kenyatta apokea ujumbe maalum kutoka Jamuhuri ya Congo

Akiongea wakati wa ufunguzi wa hospitali hiyo katika kambi ya kijeshi ya isiolo iliyoko katika kaunti ya Meru, Rais Kenyatta alisema mradi huo unaambatana na ajenda ya serikali ya utoaji huduma bora za afya kwa wote.

Rais Kenyatta alisema hospitali hiyo ni sehemu ya juhudi za kuboresha taasisi na asasi za usalama zilizoanzishwa na serikali mwaka 2013 hali kadhalika, Rais alisema serikali imeshughulikia maslahi ya maafisa wa vikosi vya usalama na familia zao kupitia ujenzi wa makazi.

Also Read
Visa 239 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa kwa upande wake alisema kuwa, wizara ya ulinzi imewekeza pakubwa katika vituo vya afya kote nchini, kuambatana na utoaji wa huduma nafuu za afya kwa wote katika ajenda nne kuu za serikali.

Also Read
Rais Kenyatta aanza ziara nchini Ushelisheli

Mkuu wa vikosi vya ulinzi hapa nchini Jenerali Robert Kibochi, alisema hospitali hiyo mpya itawahudumia vilivyo maafisa wa KDF pamoja na eneo hilo kwa jumla ambalo hapo awali halikuwa na huduma bora za afya.

Rais Kenyatta aliandamana na waziri Eugene Wamalwa wa ulinzi, mwenzake wa afya Mutahi Kagwe, Peter Munya wa kilimo pamoja na gavana wa kaunti ya Meru Kiraitu Murungi.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi