Rais Kenyatta azindua rasmi Bandari ya Lamu

Bandari ya Lamu imefunguliwa rasmi leo kwa shughuli baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuzindua awamu ya kwanza ya bandari hiyo.

Rais Kenyatta ameahidi kufungua awamu nyingine mbili za bandari hiyo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Bandari hiyo inakusudiwa kuunganisha Sudan Kusini, Ethiopia na Afrika ya Kati.

Also Read
Rais Kenyatta apokea stakabadhi za Mabalozi wapya katika ikulu ya Nairobi

Akiongea wakati wa uzinduzi wa bandari hiyo, Rais Uhuru Kenyatta amesema Bandari ya Lamu italeta mabadiliko makubwa katika kanda hii na biashara katika Bara la Afrika.

Meli mbili zilitia nanga katika bandari hiyo leo ili kuadhimisha kuanza kwa shughuli bandarini humo.

Kiongozi wa taifa aliahidi kufungua awamu nyingine mbili za bandari hiyo mwishoni mwa mwaka huu.

Also Read
Safari za ndege Kati ya Nairobi na Mombasa kusitishwa tarehe 29 mwezi huu

Kiongozi wa taifa alitoa changamoto kwa kwa viongozi wa sehemu hiyo kutafuta mikakati ya kuwavutia wawekezaji ili kuimarisha uchumi wa eneo hilo na kubuni nafasi za ajira.

Bandari hiyo inayojengwa kwa mabilioni ya pesa itaunganisha shughuli za bandari mbali mbali duniani ambazo zitaungwa mkono na kubuniwa kwa eneo maalum la kiuchumi.

Also Read
Ruto asema rekodi ya utendakazi wa serikali si jukumu lake pekee

Itatoa ajira za moja kwa moja kwa wakazi wa eneo hilo na vile vile kubuni nafasi za kazi kwa wavuvi, wasafirishaji bidhaa na biashara.

 

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi