Rais Kenyatta azindua Ujenzi wa Ulinzi Sports Complex

Rais Uhuru Kenyatta mapema Jumatano ameweka  jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo  wa Ulinzi Sports Complex wa kikosi cha Ulinzi nchini KDF  huko Lang’ata Baracks.

Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kumudu watu wapatao 10,000 na utaandaa shughuli nyingi za michezo za Kdf pamoja na  halfa nyingine za Jeshi.

Also Read
NOCK yaandaa mafunzo kwa mashirikisho ya Michezo

Kikosi cha Ulinzi hushiriki michezo mingi ikiwemo timu ya Ulinzi Stars inayoshiriki ligi kuu ya Kenya,riadha,Voliboli,uvutaji jugwe,masumbwi,uogeleaji na kadhalika.

Also Read
Ukarabati wa Kasarani kwa mashindano ya dunia waingia lala salama

Rais Kenyatta alionyeshwa ramani ya uwanja huo kabla ya kuweka jiwe la msingi ambapo kampuni ya China Wu Yi itatekeleza ujenzi huo.

Rais Kenyatta ambaye ni Amiri Jeshi mkuu alilakiwa na waziri wa Ulinzi Dkt Monica Juma na kikosi chote cha  KDF kikiongozwa na mkuu wa mwajeshi  Robert Kariuki Kibochi  kwenye hafla hiyo fupi.

Also Read
Mashindano ya riadha yahamishwa kutoka Bondo hadi Nairobi

 

 

  

Latest posts

Kocha wa Gor Mahia Andreas Spier afunganya virago

DOtuke

PSG yamfurusha Pochettino baada ya kuwa usukani kwa miezi 18

DOtuke

Timu ya taifa ya raga yanoa makali kabla ya michuano ya Jumuiya ya Madola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi