Rais Kenyatta: Covid-19 imeathiri ajenda ya kimataifa ya kuwawezesha vijana

Rais Uhuru Kenyatta amesema janga la ugonjwa wa korona limeathiri kwa muda ajenda ya kimataifa ya kuhakikisha vijana walio na umri wa kati ya miaka10 hadi 24 wanapatiwa elimu,mafunzo au ajira ifikapo mwaka wa 2030.

Akiongea Ijumaa jioni wakati wa kongamano la mtandaoni la Generation unlimited-(GenU) kuhusu uongozi,Rais Kenyatta alisema kuwa vijana wengi wamepoteza ajira na njia za kujipatia riziki,huku wengine wakiangukia kwenye masaibu ya uraibu wa pombe,utumizi wa mihadarati na mimba za mapema.

Also Read
Watu 376 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Alisema vijana wengi waliathiriwa hasa wakati shule zilipofungwa kwa muda kutokana na janga la Covid-19.

Hata hivyo alisema licha ya tatizo hilo vijana wamekuwa na ubunifu mpya ambao unafanya kongamano hilo kudumisha maana na umuhimu wake.

Also Read
Sonko afikishwa mahakamani Kiambu na kukanusha mashtaka ya kuzua vurugu

Alitaja mfano wa kijana Calvin Shikuku Odhiambo, kutoka Kenya aliyeshinda tuzo ya mwaka 2020 ya GenU, baada ya kubuni vipumulio vilivyomfanya kutambuliwa na Umoja wa mataifa kuwa mtu mashuhuri wa mwaka.

Also Read
Maendeleo Chap Chap chajiondoa kwenye uchaguzi mdogo wa Seneta wa Machakos

Rais Kenyatta alisisitiza haja ya vijana kupewa fursa ya kudhihirisha vipaji vyao,akisema wao ndio walio na uwezo wa ubunifu na udumishaji wa mikakati ya mkakati huo wa GenU.

Kiongozi wa taifa alitaka vijana kushirikiana kupitia mitandao na kuhimiza ujasiriamali na maarifa mapya miongoni mwa vijana ili kuleta mabadiliko.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi